Mwanamke Tajiri Ajilipua kwa Harmo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwanamke Tajiri Ajilipua kwa Harmo


HUWENDA ziara ya kimuziki ya msanii mwingine mkubwa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul au Harmonize huko nchini Marekani, imeanza kutoa matokeo mengine mapya, Gazeti la IJUMAA limedokezwa.

Taarifa ikufikie kwamba, kuna mwanamke mmoja tajiri wa kutupwa; mwenye pesa kama vumbi huko Marekani anayetajwa kwa jina la Christine Lewis, anadaiwa kujilipua ‘live’ kwa kummwagia mamilioni Harmonize au Konde Boy Mjeshi.

AMUALIKA KWENYE BIRTHDAY

Kwa kutambua uwepo wa Harmonize au Harmo nchini Marekani akiendelea na ziara zake kabambe za kimuziki, mwanamama huyo alimualika nyumbani kwa ajili ya kupafomu kwenye birthday ya binti yake aliyetimiza umri wa mwaka mmoja.

MILIONI 160 ZATUMIKA

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Kenya ambapo mwanamama huyo ana asili ya nchini humo na anafahamika kwa undani zaidi, alitumia kiasi cha shilingi milioni 7.8 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 160 za Kitanzania kwa ajili ya mwaliko wa Konde Boy Mjeshi na pati nzima ya mwanawe iliyodumu usiku kucha.

NI SINGO-MAMA WA WATOTO WATANO

Christine Lewis anatumia jina la @itsabossmom kunako Mtandao wa TikTok ambapo anajitambulisha kama singo-mama wa watoto watano kama ilivyo kwa mwanamama Zari The Boss Lady ambaye naye ni mama wa watoto watano, lakini bado anaita.

Pia Christine Lewis anajitambulisha kama muasisi wa shughuli za kujitolea misaada kwa jamii (philanthropist).

Lakini vyovyote itakavyokuwa, baadhi ya watu wanaomjua Christine Lewis wanasema ni mama bora kabisa anayependa kuishi maisha ya kifahari (lavish life kama Zari) na kufanya kila liwezekanalo kuwafurahisha wanawe kama huyo ambaye alikuwa anatimiza umri wa mwaka mmoja na mburudishaji ni Harmonize hivyo inaweza kuwa ‘koneksheni’ nzuri kwa jamaa huyo anayepeperusha vizuri bendera ya muziki wa Bongo Fleva kimataifa.

Kwenye pati hiyo, Harmonize alikodiwa mahsusi kwa ajili ya kupafomu wimbo wake wa Happy Birthay ikiwa ni kama zawadi kwa mtoto huyo.

MWANAMKE AFUNGUKA

Akifunguka kupitia Mtandao wa TikTok juu ya uwepo wa Harmonize kwenye pati hiyo ya mwanawe, Christine Lewis anamshukuru kwa furaha aliyoiweka kwenye familia yake akisema; “Ndiyo, Harmonize alikuwepo kwa ajili ya kupafomu kwa ajili ya mtoto wangu wa kike na wageni wake.

“Ni kweli ilikuwa ni ghali, nilitumia Dola za Kimarekani 78,000 (sawa na shilingi za Kenya milioni 7.8; zaidi ya shilingi milioni 160 za Kitanzania) kwa ajili ya mwanangu…”

NI MKENYA AISHIE MAREKANI

Kwa mujibu wa wanaomjua mwanamama huyo wanasema kuwa, ni Mkenya aishie nchini Marekani kama ilivyo kwa Zari ambaye ni Mganda aishie nchini Afrika Kusini.

Imefahamika kwamba, Christine Lewis ni daktari wa binadamu anayefanyia kazi zake nchini Marekani.

Wanasema ni mama wa watoto watano na ana utajiri kama alivyo Zari kutokana na maisha ya kifahari anayoishi.

SIYO WATU NJAA

Video za tukio hilo la birthday zinamuonesha Harmonize akipafomu wimbo wake wa Happy Birthday na wahudhuriaji wa pati hiyo wakionekana kabisa kwamba siyo watu wa njaa.

Harmonize ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Music baada ya kufanya shoo kwenye Miji ya Columbus, Ohio, Houston, New York na Idaho, Minnesota sasa ataendelea kukiwasha huko Los Angeles, Las Vegas, Syracuse kisha atarejea New York kwa mara nyingine.

Hata hivyo, baadhi ya shoo za Konde Boy Mjeshi zilishindwa kuendelea huko Canada na Bara la Ulaya kutokana na majanga ya maambukizi ya UVIKO-19, lakini shoo zake nyingine za kimataifa zitaendelea hadi Januari, mwakani.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz