Azam FC yafungasha virago michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Azam FC yafungasha virago michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika
Klabu ya Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Pyramids bao pekee la Ally Gabri Mossad dakika ya 29 usiku wa jana Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo, Misri.

Hiyo inafuatia Azam FC kulazimishwa sare ya 0-0 na timu hiyo ya Misri katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Sasa Pyramids itamenyana na moja ya timu zitakazotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz