Mchongo wa Rosa Ree na Profesa Jay Upo Hivi Yaani - EDUSPORTSTZ

Latest

Mchongo wa Rosa Ree na Profesa Jay Upo Hivi Yaani


Msanii wa Bongofleva anayefanya vizuri katika Hip Hop, Rosa Ree tayari ameshazungumza na Mkongwe wa muziki huo, Profesa Jay kwa ajili ya kufanya kazi pamoja jambo ambalo limekuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Kauli ya Rosa Ree inakuja mara baada ya wawili hao kuonekana pamoja kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki wengi kuhoji iwapo wapo katika mchakato wa kufanya kazi pamoja.

Rosa Ree amesema Profesa Jay amekuwa kama Baba kwake kimuziki kutokana na mchango wake wa kuikuza Bongofleva, hivyo kufanya naye wimbo itakuwa ni hatua kubwa kwake.

"Kifupi ni msanii ambaye namkubali, namuheshimu sana na ningependa kufanya naye kazi sana, na ni kitu ambacho nimeshamwambia mara nyingi, na Mwenyenzi Mungu akipenda tutaweza kufanya na mashabiki wataisikia," amesema.

"Ni ambaye wote tunampenda, tumekuwa tukimtazama, tukiangalia nyimbo zake, nimejifunza mambo mengi kutoka kwake hasa mimi kama msanii, huwa namuitwa Baba na wasanii wengine kwa sababu alitutangulia kwa kuchonga barabara ambayo imenyooka katika muziki kwa ajili yetu," amesema Rosa Ree.

Ikumbukwe tayari Rosa Ree amefanya kazi na wasanii wa Hip Hop kama Fid Q, G Nako, Billnass na Khaligraph Jones kutokea nchini Kenya.

UswazTv
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz