Makubwa.. Mpiga Picha Afuta Picha za Maharusi Baada ya Kunyimwa Chakula Harusini - EDUSPORTSTZ

Latest

Makubwa.. Mpiga Picha Afuta Picha za Maharusi Baada ya Kunyimwa Chakula HarusiniAkitoa malalamishi yake kupitia mtandao wa Reddit, tuvuti maarufu ya Marekani, mpiga picha huyo alikuwa amekodishwa na rafiki yake ambaye alikuwa na sherehe ya harusi ampige picha.

Alisema huduma zake hazijawahi kukodishwa mbeleni na bwana harusi huyo alimtafuta sababu ya gharama yake ya chini.

Mpiga picha huyo baada ya kushawishiwa, aliamua kuchukuwa kibarua hicho na kuwasili mapema katika harusi ya swahiba wake kuchapa kazi.


Akiwa amejihami na vifaa vyake, alianza kazi saa tano asubuhi na alikuwa ameratibiwa kumaliza kufikia saa moja usiku.

Raila Awaahidi Wakenya Kuwa Bei ya Mafuta Itashuka Wiki Ijayo
Katika hafla hiyo, wakati wa chakula uliwadia na kila mgeni alikuwa akipakuliwa.

Mpiga picha huyo alijaribu kujumuika na wengine kwa chakula lakini alizuiwa na bwana harusi akihoji kuwa anatakiwa kupiga picha ya hafla nzima bila kusita wala kupumzika.

STORI ZAIDI za AINA HII Download Udaku Spesho App HAPA

Alisema alikuwa amechoka tiki, na kile alihitaji ni kupumzika na angalau kupata kopo la maji ambalo alinyimwa.

Bwana harusi alimtishia kuwa hatamlipa iwapo atapumzika.

“Nilimwambia bwana harusi kuwa nahitaji kupumzika kwa dakika 20 angalau kupata chakula na maji.Lakini bwana harusi aliniambia kuwa natakana kuwa mpiga picha ama niondoke bila kulipwa," aliandika mpiga picha huyo.

Mpiga picha hiyo alikasirika na kumuomba bwana harusi iwapo anaweza kufuta picha zote ambazo alikuwa amezipiga siku hiyo.


Bwana harusi alikubali na kisha mpiga picha huyo alifuta picha zote kabla ya kuondoka akiapa kutowahi kujihusha tena na hafla za bwana harusi huyo.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza HAPA

Alisema pesa ambazo alikuwa anatazamia kulipwa zilikuwa kidogo na za kudunisha thamani yake.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz