Samatta asepa bongo, awashukuru Watanzania - EDUSPORTSTZ

Latest

Samatta asepa bongo, awashukuru Watanzania

MZAWA Mbwana Samatta na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania,  muda mfupi baada ya kunaliza kazi ya kukiongoza kikosi cha Tanzania katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia alikwea pipa.


Samatta alikuwa ni nyota kwenye mchezo wa jana uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ubao ukasoma Tanzania 3-2 Madagascar. Ni pasi ya mwisho ya ushindi alitoa kwa Feisal Salum ambaye hakuifanyia  makosa aliijaza kimiani kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango.Anakwenda kwenye majukumu ya timu yake ya sasa ya Antwerp FC atakayokuwa huko kwa msimu huu  wa 2021/22.Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Asante wachezaji kwa kupambana, benchi la ufundi kwa maelekezo mazuri, Watanzania kwa dua njema, kwa kheri ya kuonana Tanzania, ".


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz