elru87tYGBGEm Ndoa ya Zabibu Kiba Yadaiwa Kuvunjika - EDUSPORTSTZ

Latest

Ndoa ya Zabibu Kiba Yadaiwa Kuvunjika

MIAKA kadhaa imepita tangu dada wa staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Ali Saleh Kiba au King Kiba aitwaye Zabibu Kiba afunge ndoa na aliyekuwa msakata kabumbu wa Klabu ya Hilands Parks ya nchini Afrika Kusini, Abdi Banda, lakini sasa ndoa hiyo inadaiwa kuingia kidudu mtu.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mtu wa karibu KABISA na familia ya Zabibu ambaye ameomba hifadhi ya jina, anadai kuwa, amesikia ndoa ya wawili hao imevunjika huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni mwigizaji wa Bongo Movies, Husna Sajent.

 

“Ni hivi, inasemekana mwanaume anatoka kimapenzi na Husna; yule dada wa Bongo Movies, tena wana muda mrefu tu na wameshaonekana mara kadhaa wakiwa pamoja.“Yaani bila hata aibu nasikia huyo Husna huwa anamfuata mume wa mtu hadi mazoezini, sasa baada ya Zabibu kupata hizo habari, nasikia ndiyo alichukia hadi kusababisha ndoa yao ikaingua doa,” anasema mtu huyo.


Gazeti la IJUMAA, kama kawaida yake huwa halilazi damu hivyo limemtafuta Husna ili kupata ukweli wa jambo hilo akiwa kama mshukiwa, lakini cha kushangaza baada ya kusomewa mashitaka yake alikuwa mkali na kumtaka mwandishi amuache.


IJUMAA: Mambo vipi Husna?
HUSNA: Poa…
IJUMAA: Unaongea na Mwandishi wa
Gazeti la IJUMAA hapa…
HUSNA: Karibu…


IJUMAA: Asante, hivi ni kweli kwamba unatoka kimapenzi na mume wa mtu ambaye inasemekana ni Banda?
HUSNA: (anakuwa mkali) Heheheee! Jamani naomba tuongelee kuhusu kazi zangu tafadhali…
IJUMAA: Hujanijibu kama tuhuma hizo ni za kweli au la…


HUSNA: Tafadhali nina kazi zangu (anazitaja) naomba tuziongelee hizo na siyo hayo mambo mengine (kisha anakata simu)…Baada ya Gazeti la IJUMAA kutoridhishwa na majibu ya Husna lilimsaka Zabibu ambaye naye kwa upande wake mambo yalikuwa hivi;
IJUMAA: Mambo vipi Zabibu?
ZABIBU: Poa, mambo?


IJUMAA: Safi, nina imani unajua
unazungumza na nani, kuna habari hapa kwamba ndoa yako na Banda hali si shwari, eti Husna na mwanadada mwingine anayesemekana anafanya kazi hospitali moja iliyoko Msasani ndiyo chanzo, hizi taarifa zina ukweli kiasi gani, maana hata sisi zimetushtua?
ZABIBU: Na mimi nimezisikia…


IJUMAA: Sasa unalizungumziaje suala hilo?
ZABIBU: Nawaombea kila la heri, kuanzia huyo Husna hadi huyo mwingine wa Msasani wadumu na mahusiano yao…
IJUMAA: Lakini huoni kama wanashusha hadhi yako?


ZABIBU: Hawawezi kwa sababu siko kwenye skendo yao, hapo ni wao na
siyo mimi.
IJUMAA: Kwa hiyo ni kweli kwamba ndoa yako na imevunjika kwa sababu yao?
ZABIBU: Sijui…


IJUMAA: Una maana gani kusema hujui?
ZABIBU: Hawawezi wao kuwa sababu kwenye maisha yangu kwa chochote.
IJumaa: Kivipi? Hebu fafanua kidogo.
Zabibu: Asante, karibu tena.Zabibu na Banda walifunga ndoa Agosti Mosi, 2018 ambapo hadi sasa wamejaaliwa mtoto mmoja wa kiume.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz