Mtoto wa Monalisa Aliyesema Havijui Vyuo vya Tanzania Aenda Kusoma Chuo Nchini Ukraine - EDUSPORTSTZ

Latest

Mtoto wa Monalisa Aliyesema Havijui Vyuo vya Tanzania Aenda Kusoma Chuo Nchini UkraineMtoto wa Msanii wa filamu Bongo, Monalisa, Sonia ameenda kusoma Chuo Kikuu cha Summy State nchini Ukraine.

Sonia anakwenda kusomea kozi ya Uhasibu na Ukaguzi (Accounting and Auditing) kwa kipindi cha miaka minne. 

"Sababu ya kuchagua kwenda kusoma nchi hiyo ni kwanza wametutangulia kiteknolojia kwa hiyo tunapoenda huko kusoma tunaweza hamisha teknolojia kwa njia ya elimu kuja hapa Tanzania"

"Kitu kingine Ukraine na Urusi ni nchi ambazo zina fursa nyingi za utalii hivyo tunavyoenda huko kusoma ni nafasi yetu kuwaambia Tanzania kuna nafasi nyingi za Uwekezaji, kuna Mlima Kilimanjaro, Tanzanite na mengine mengi ambayo Tanzania tunajivunia" amesema Sonia.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz