Msimchukulie Poa Msanii Marioo Aangaliwe kwa Jicho la Tatu..Sio Rahisi - EDUSPORTSTZ

Latest

Msimchukulie Poa Msanii Marioo Aangaliwe kwa Jicho la Tatu..Sio Rahisi


Aisee @marioo_tz ni genius wa muziki wa bongo, Nyimbo za vilio vya mapenzi yuko poa. Sikiliza Inatosha na Unanionea utanielewa. Nyimbo za kuruka sikiliza Mama Amina, Beer, Nyimbo za kufurahia penzi sikiliza For You.

Huyu jamaa atafika mbali sana narudia tena kusema hili. Naiona nidhamu ya hali ya juu kwa management yake na ana mashairi ya peke yake na midundo inafanya muziki wake usikuchoshe kuusikiliza.

@marioo_tz ni level nyingine, cha msingi tu watu wabaya wasije wakamfanyia figisu. Maana wakati wanafanya mabifu kati ya Mondi, Kiba na Harmo wanasahau kuna Marioo njia yake inazidi kuwa nyeupe anapita bila upinzani on the way to the top.

Yote kwa yote @marioo_tz anajitahidi kutembea na soko. kutusua enzi hizi za @diamondplatnumz ni ngumu sana. Lakini dogo amejitahidi kupenya mpaka kufikia hapo alipo. Naamini akizidisha bidii na kuendelea kutulisha kitu masikio inapenda, atakuwa star mkubwa wa hapo mbele.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz