Msanii Young Lunya Afunguka Kuhusu Kutoka Kimapenzi na Irene Uwoya "Ni Mwanamke Mzuri" - EDUSPORTSTZ

Latest

Msanii Young Lunya Afunguka Kuhusu Kutoka Kimapenzi na Irene Uwoya "Ni Mwanamke Mzuri"


Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Young Lunya amekanusha madai ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Muigiza Irene Uwoya.

Lunya amesema kama ingekuwa ni kweli angeweka wazi hilo kutokana Irene ni mwanamke mrembo.

"Sijawahi kuwa na mahusiano na Irene Uwoya, labda watu wanahisi itapendeza zaidi mimi nikiwa naye. Unajua yule ni msichana mzuri sana"

"Mimi siwezi kukata kusema sitoki na Irene Uwoya kwa sababu kwani ana tatizo gani?, ni mwanamke mzuri sana, kwa hiyo ingekuwa natoka naye nisingeweza kukataa," amesema Lunya.

Utakumbuka Young Lunya ni miongoni mwa wasanii watatu wanaounda kundi la OMG Tanzania, wengine ni Salmin Swaggz na Conboi.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz