Kunani..Rayvanny Ashindwa Kumtambulisha Paula UKWENI..Aenda Mbeya Peke yake - EDUSPORTSTZ

Latest

Kunani..Rayvanny Ashindwa Kumtambulisha Paula UKWENI..Aenda Mbeya Peke yake
MIONGONI mwa maswali yanaulizwa kwenye vilinge vya ubuyu mtamu ni kwa nini Rayvanny amekwenda nyumbani kwao jijini Mbeya bila kwenda na mpenzi wake Paula?

Inafahamika kwamba Rayvanny hivi karibuni alikwenda kufanya balaa kwenye Tamasha la Ngoma za Asili maarufu kama Tulia Traditional Dance lililoandaliwa na viongozi chini ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson katika Jiji la Mbeya.

Pia inafahamika kwamba Rayvanny ni mwenyeji wa Mbeya hivyo tangu alipotua uwanja wa ndege Mbeya kila shabiki alikuwa anaulizia yupo wapi Paula, lakini jamaa huyo hakuwa na jibu.

Tofauti na alivyofanya kwa Fahyma alipokwenda kumtambulisha kwa wazazi wake, lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Baadhi ya watu wa karibu wa Paula wanamuambia kwamba, kuna shida kwani mbona alisafiri naye kwenda kwenye shoo Zanzibar na Naironi, kwa nini ameshindwa kwenda naye nyumbani kwao Mbeya?

Kwenye mjadala huo, Rommy Jons ambaye ni Makamu wa Rais wa Wasafi alimshauri Rayvanny; “Muoe tu au mpe mimba kama Fahyma halafu atulie…”

Hata hivyo, wenyewe wameendelea kupostiana kwenye kurasa zao za Instagram huku Paula akilalamika kwamba siku hizi jamaa huyo hampigii simu kumtakia usiku mwema kama ilivyokuwa zamani.

Tangaza Biashara yako nasi Piga simu 0714604974
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz