Jamaa mmoja anaripotiwa kujitoa uhai katika mtaa wa Umoja usiku wa Jumamosi kufuatia mzozo wa kinyumbani.
Marehemu ambaye ametambulishwa kama Brayo (29) anasemekana kuzozana na mkewe kuhusiana na suala lisilojulikana kabla ya kufanya maamuzi ya kunywa sumu iliyokatiza maisha yake.
Kulingana na DCI, hapo awali mke wa Brayo alikuwa ametishia kuacha ndoa yao na marehemu akajaribu kumuomba asimuache.
Licha ya juhudi za Brayo kushawishi mpenzi wake asiondoke, mwanadada huyo anadaiwa kuchukua vitu vyake na kurudi nyumbani kwa wazazi wake katika mtaa wa Dandora.
Usiku huo jamaa huyo ambaye alikuwa amejawa na masikitiko kufuatia yaliyokuwa yametukia alimtumia mkewe ujumbe ambao uliosema "nimekuachia dunia".
Baada ya kusoma ujumbe ule, mwanadada huyo alijaribu kumpigia mumewe simu mara kadhaa ili amshawishi asijitie kitanzi ila simu ila juhudi zake ziliangulia patupu kwani simu zake hazikuchukuliwa..
Asubuhi ya Jumapili mwanamke huyo aliandamana na ndugu ya marehemu kuelekea kwa nyumba yake ili wakamjulie hali ila wakapigwa na butwaa kupata mwili wake ukiwa umelala kitandani.
No comments:
Post a Comment