Ethiopia yatangaza mpango wa kuanza kutumia tena ndege aina ya Boeing 737 Max - EDUSPORTSTZ

Latest

Ethiopia yatangaza mpango wa kuanza kutumia tena ndege aina ya Boeing 737 Max





Shirika la ndege la Ethiopia linajiandaa kutumia tena ndege aina ya Boeing 737 Max iliyoanguka mnamo Machi 10, 2019 baada ya kuruka kutoka Addis Ababa kwenda mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika ya ndege ya Ethiopia Tewolde Gebremariam,, alisema kwamba ndege aina ya Boeing 737 Max itaanza tena kutumika mwanzoni mwa mwaka ujao.

Gebremariam alisema kuwa baada ya mipango hiyo, waliamua kuwa ndege hiyo ilikuwa salama.

Shirika la ndege la Ethiopia na Boeing walitia saini hati ya makubaliano katika nyanja mbalimbali kama vile maendeleo ya viwanda na elimu mwishoni mwa Agosti.

Baada ya Boeing 737 Max 8 kuanguka nchini Indonesia mnamo 2018 na Ethiopia mnamo 2019, nchi nyingi ziliacha matumizi ya ndege hiyo.

Shirika la utengenezaji wa ndege la Marekani la Boeing, ambalo liliomba radhi kwa wale waliopoteza maisha katika ajali, lilisasisha programu ya Maneuvering Characteristics Reinforcement System (MCAS) ya ndege aina 737 Max.

Watu 157 walifariki katika ajali ya ndege iliyoanguka baada ya kuruka kutoka Addis Ababa kwenda mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya mnamo Machi 10, 2019.






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz