elru87tYGBGEm Basi la mwendokasi lagonga pikipiki, laua wawili - EDUSPORTSTZ

Latest

Basi la mwendokasi lagonga pikipiki, laua wawili

Dar es Salaam. Watu wawili wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha basi la mwendokasi na pikipiki.


Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Septemba 8, 2021 saa 3:20 usiku.


Amesema ajali hiyo imetokea katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari.


Ameitaja pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan (17), Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.


“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa pikipiki kutii sheria za usalama barabarani hususani taa za kuongozea magari, kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za Mwendokasi,” amesema Muliro.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz