Yanga kuwaita wachezaji wake walipo kambi ya Taifa stars - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuwaita wachezaji wake walipo kambi ya Taifa stars






U ONGOZI  wa  Yanga umesema  kuwa utawaita  wachezaji wote  wa timu hiyo ambao wapo  kambini kwa sasa kwenye  timu ya taifa ya Tanzania  kwa ajili ya mchezo wa  kufuzu Kombe la Dunia kuja  kuhudhuria katika kilele cha  Wiki ya Mwananchi.


Timu ya Taifa ya Tanzania iliingia kambini Agosti 25, tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya DR Congo utakaofanyika Septemba 2, nchini DR Congo.



Wachezaji Yanga ambao wameenda kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania ni Feisal Salum, Dickson Job, Zawadi Mauya na Ramadhani Kabwili.

 


 Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro, alisema kuwa tayari wameshawasiliana na uongozi wa timu ya taifa juu ya kuwaomba wachezaji hao kwa ajili ya kuja kushiriki Siku ya Mwananchi kisha kurejea tena kambini.



“Tayari tumeshaongea na uongozi wa timu ya taifa ya Tanzania juu ya kuwaomba wachezaji wetu wote katika mchezo wa kilele cha siku ya Mwananchi dhidi ya Zanaco FC na tayari ombi letu limekubaliwa.

 


“Hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi juu ya kuwakosa wachezaji hao na kilichobaki kwa sasa mashabiki wanatakiwa wafike kwa wingi kwani kutakuwa na mambo mengi mazuri kwa ajili yao,” alisema kiongozi huyo.

 






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz