Waandamana kupinga chanjo ya corona, - EDUSPORTSTZ

Latest

Waandamana kupinga chanjo ya corona,

 
Maelfu ya watu wanaopinga kupigwa chanjo wameandamana katika miji miwili ya Ugiriki hapo jana wakilalamikia masharti makali yaliyotangazwa kwa lengo la kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.



Miongoni mwa sheria mpya ni kwamba watu ambao hawakuchanja hawatoruhusiwi kuingia migahawani na kuanzia Septemba mosi wahudumu wa afya ambao waliogoma kuchanjwa watafukuzwa kazi bila ya malipo.

Greek police fire tear gas as 7,000 protest coronavirus vaccine rules,  Europe News & Top Stories - The Straits Times

Vyombo vya habari vimekisia kwamba watu wapatao 3,000 waliandamana mjini Athens na wengine zaidi ya 5,000 waliandamana katika mji wa kaskazini wa Thessaloniki.



Karibu na maandamano hayo kumalizika mjini Athens, watu wapatao 200 walianza kuwarushia mawe polisi nje ya jengo la bunge.

Na polisi waliwatawanya kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi, na maji ya kuwasha. Serikali ya Ugiriki imelazimika kutangaza masharti makali kwani maambukizi yameongezeka hivi karibuni kutokana na kwamba ni kipindi cha likizo barani Ulaya.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz