Tanzia: Nyota Mtibwa Sugar Afariki - EDUSPORTSTZ

Latest

Tanzia: Nyota Mtibwa Sugar Afariki




MADILU Mosha, aliyekuwa mchezaji wa Klabu ya Vijana ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ametangulia mbele za haki.

 

Taarifa rasmi iliyotolewa na Mtibwa Sugar kupitia Ukurasa rasmi wa Instagarm leo Agosti 3, 2021 imeeleza:”Timu ya Mtibwa Sugar pamoja na uongozi wake umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa mchezaji wa timu ya vijana Madilu Mosha.

 

“Tunaungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu. Tunaomba Mungu awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Ameen,”.

Pumzika kwa amani mwanafamilia ya michezo.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz