Simu 10 zinazoongoza kwa mauzo zaidi Afrika - EDUSPORTSTZ

Latest

Simu 10 zinazoongoza kwa mauzo zaidi Afrika



Haitokuwa ngumu kujua ni chapa(Brand) gani au Simu gani ambayo inauza sana Duniani,kutoka kwenye vyanzo tofauti tofauti vinasema chapa za kampuni ya Apple(iPhone)ndio bado zinaongoza katika uuzaji wa simu Duniani kote ikifuatiwa na Samsung ambayo inashika nafasi ya pili.



 

Ila cha kushangaza simu hizo mbili ambazo ndio zinaongoza kwa kuuzika Duniani hazija shika nafasi ya kwanza kwa kuuzika Afrika, Simu inayoongoza kwa kuuzika Afrika ni”TECNO” hicho ndio kilicho fanya wengi kushangaa na katika orodha ya Simu kumi bora zilizo uza sana duniani chapa(Brand) au Simu za”TECNO”hazipo,ila kwa Afrika ndio chapa(Brand)inayongoza kwa kuuzika

Hali ina utofauti kidogo kwa Afrika kutokana na uwezo wa kipato kwa Wafrika wengi kuwa ni wa hali ya chini,hivyo ndio maana ikawa rahisi kwa chapa(Brand)za Kampuni ya”TECNO” kushika nafasi ya 1 Afrika katika masoko kutokana na Bei zao kuendana na kipato cha Wafrika wengi kulinganisha na Simu za Apple na Samsung ambazo zina gharama katika ununuzi wake,Japokuwa Makampuni mengi yaliyumba kiuchumi kutoka na janga lilliloikumba Dunia kwa Ugonjwa wa UVIKO-19(COVID-19),ila chapa(Brand) ya “TECNO” haikuweza kuyumba sana iliendelea kutengeneza bidhaa kulinganisha na Makampuni mengine na huwenda hiyo ndio ikawa sababu ya chapa(Brand) za “TECNO” kuwa namba moja Afrika,

Hii ndio orodha ya Simu (10) zilizouza sana Afrika kwa mwaka 2020
1)TECNO
2) SAMSUNG
3)ITEL
4)HUAWEI
5)INFINIX
6)XIAOMI
7)OPPO
8)APPLE
9)NOKIA
10)REALME

Source (www.moshekafrica.com)





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz