Simba Day Rasmi Kufanyika Septemba 15 - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba Day Rasmi Kufanyika Septemba 15


BAADA ya kuwepo kwa uvumi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutofanyika kwa tamasha la siku ya Simba ‘Simba Day’ Uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kuweka wazi kuwa tamasha hilo lipo, huku taarifa za ndani zikieleza kuwa kuna uwezekano mkubwa tarehe rasmi ya kufanyika kwa tamasha hilo ikawa ni Septemba 15, mwaka huu.


Kwa kawaida tamasha hilo hufanyika Agosti 8, kila mwaka ambapo kwa mwaka huu uongozi wa Simba ulilazimika kulisogeza mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ratiba ngumu ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’.

 

Sehemu kubwa ya kikosi cha Simba kwa sasa kipo nchini Morocco kwa ajili ya kambi ya kabla ya msimu ambayo inatarajiwa kuendelea mpaka mwishoni mwa msimu, huku nyota wengine 12 wakiwa wameitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa.Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia gazeti hili kuwa ratiba ya awali ya tamasha hilo inaonyesha linatarajiwa kufanyika Septemba 15, mwaka huu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, kuhusu tamasha hilo Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu alisema:

 

“Kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wakijaribu kusambaza uvumi kuwa eti tamasha letu la ‘Simba Day’ lisingekuwepo mwaka huu kwa sababu mbalimbali ambazo wamezieleza, lakini nikuhakikishie kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

 

“Kwa sasa menejimenti inapanga utaratibu mzima wa kufanyika kwa tukio hilo, na tutatoa taarifa rasmi juu ya utaratibu mzima wa kufanyika kwa tamasha hilo.”


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz