Ndoa ya Paula na Rayvanny Yakataliwa Mtandaoni - EDUSPORTSTZ

Latest

Ndoa ya Paula na Rayvanny Yakataliwa Mtandaoni
BIG no! Moja kati ya stori zilizotikisa kwa sasa ni tangazo la ndoa ya staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na mchumba’ke, Paula Paul au Paula Kajala ambayo imekataliwa kila koja, IJUMAA limedokezwa.
Mapema wiki hii, wawili hao walikwenda mbali zaidi na kuposti maneno yaliyoashiria uwepo wa ndoa yao siku si nyingi zijazo.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny au Chui aliposti picha ya mpenzi wake huyo na kusindikiza na emoj za upendo kisha baadaye akaandika tena ujumbe kwenye Insta Story yake uliosomeka; “Can’t wait for my wedding…” (Sijui itakuwaje siku ya ndoa yangu).Kauli hiyo ilionekana kuwaibua Team Fahyma ambaye ni baby mama wa jamaa huyo ambapo wengi walidai kuwa, kamwe Rayvanny hawezi kumuoa Paula kwa sababu bado hajamaliza starehe zake hivyo atamtumia tu kwa kumdanganyadanganya kisha mwisho wa siku amuache na kurudi kwa mke wake.

 

“Yaani namuonea sana huruma Paula, bado ni mdogo maskini, hayajui mapenzi, kuna siku Rayvanny atakuja kumuacha vibaya, aumie kama alivyoumizwa Fahyma, hakuna ndoa hapo labda ya ndotoni,” anasema shabiki mmoja aliyefahamika kwa jina la Maggie aiungwa mkono na wafuasi wengi ambao wameungana kuipinga ndoa hiyo.“

 

Ndoa Bongo! Huyo Rayvanny alishindwa kumuoa Fahyma na uzuri wake wote ule, aje amuoe Paula aliyekutana naye juzi, hakuna kitu kama hicho, hapo anamdanganya tu ili aendelee kumchezea na yeye anakubali,” shabiki mwingine alichangia mjadala huo ambao umevuta hisia za wengi.

 

Gazeti la IJUMAA limezungumza na mmoja wa watu wa karibu na familia ya Paula ambapo alisema kuwa, ni kweli Rayvanny ana mpango wa kumuoa Paula kwa hiyo watu wakae mkao wa kutulia kwani kila kitu kitakuwa sawa.

 

“Unajua sisi tunawashangaa sana watu wanaoongea mambo yasiyowahusu, Rayvanny ana mpango wa kumuoa jumla Paula na hii anafanya kwa sababu anampenda na hataki kumpoteza, kwa hiyo watu wakae kwakutulia,” anasema mtu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini kwa kumuhofia mama wa Paula, Kajala Masanja.

 

Miaka kadhaa iliyopita, Rayvany aliingia kwenye penzi zito na Fahyma ambaye ni mwanamitindo maarufu Bongo hadi wakafikia hatua ya kuzaa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydany.

 

Hata hivyo, baadaye penzi lao liliingia doa baada ya staa huyo kudata na penzi la mtoto mbichi, Paula ambaye ndiye yupo naye hadi sasa.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz