Manara: Senzo Alipewa Kazi ya Kunifukuza, Barbara Amewafukuza Wote - EDUSPORTSTZ

Latest

Manara: Senzo Alipewa Kazi ya Kunifukuza, Barbara Amewafukuza Wote

ALIYEKUWA msemaji wa Simba, Haji Manara  leo Agosti 4, 2021 amedai kuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Babara ndiye amekuwa kinara wa kuwaondoa watu wote waliohusika na mabadiliko ya Simba.

 

“Barbara huyu anasema Kashembe anahujumu Simba? Kashembe huyu aliehusika kwenye transformation? Kifupi watu wote muhimu walioapambana transformation ipite leo hii wanaonekana hawana maana, Barbara huyo.

 

“Kila anaeondoka Simba tu basi sababu ni kuhujumu, wameondoka zaidi ya watu 12 kwa kosa moja, mara Mbaga, mara Senzo na sasa Haji kaondoka, haya yote yapo chini ya Barbara ndie muhusika mkuu wa yote.

 

“Wakati Senzo anakuja kwa mara ya kwanza, alinifuata na kuniambia amepewa kazi ya kunifukuza Mimi kazi, lakini Senzo alihoji kwanini nimfukuze bila sababu?

 

“Kifupi walimleta ili atekeleze matakwa ya wakubwa ila Senzo alisimama imara sana, alipinga kufanya kitu bila kukichunguza ndicho kilichomuondoa Simba,” Haji Manara.

 
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz