Kumekucha..Mkuu wa Shule aonywa kwa kumkaribisha Amber Rutty kuwa mgeni rasmi - EDUSPORTSTZ

Latest

Kumekucha..Mkuu wa Shule aonywa kwa kumkaribisha Amber Rutty kuwa mgeni rasmi​​​​​​​UONGOZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke umeonesha kuchukizwa na kitendo cha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nzasa cha kumualika Amber Rutty kuwa kama mgeni rasmi na kuongea na Wanafunzi.

“Kumekua na taarifa zinazosambaa kupitia kipande cha video mitandaoni zikimuonesha mtu mmoja akitembelea Shule ya Msingi Nzasa iliyopo Temeke, akiwa amevaa mavazi yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania”

“Tunapenda kutoa taarifa kwamba uongozi wa Manispaa ya Temeke umechukizwa na ugeni huo, umemuonya Mkuu wa Shule kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kutokana na kitendo kilichotokea na Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza” kimesema Kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Temeke.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz