Kortini wakidaiwa kusafirisha Watanzania 90 kwenda Canada na Mauritius - EDUSPORTSTZ

Latest

Kortini wakidaiwa kusafirisha Watanzania 90 kwenda Canada na Mauritius
Dar es Salaam. Raia wa Misri, Mohamed Morsy Shalaby (52) na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kusuka mpango wa kusafirisha binadamu.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwasafirisha watu 95 kati yao Watanzania wakiwa 90 na raia watano wa Burundi kwenda nchini Canada na Mauritius.

Mbali na Shalaby, washtakiwa wengine ni Ally Rajabu(40) Mtanzania na mkazi wa Kariakoo pamoja na Chebet Benson(33) raia wa Uganda.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani leo Jumanne Agosti 10, 2021 na kusomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka kutoka Idara ya Uhamiaji, Godfrey Ngwijo akisaidiana na Sitta Shija mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Godfrey Isaya.

Wakili Ngwijo amedai washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 132/2021 kwamba shtaka la kwanza la kusafirisha binadamu linamkabili Shalaby anayedaiwa kulitenda Agosti 4, 2021 katika nyumba za makazi za Avone zilizopo

Ilala akidaiwa kuwa na alikutwa na watu 95.


Shtaka la pili ni kuandaa na kupanga mpango wa usafirishaji haramu wa binadamu linalomkabili Rajabu anayedaiwa kulitenda maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Shtaka la tatu ni kufanya kazi nchini bila kuwa na kibali linalomkabili Benson anayedaiwa kutenda kosa hilo Agosti 4, 2021 katika hospitali ya Sali iliyopo Masaki.

Hata hivyo,  mshtakiwa Rajabu amekiri shtaka linalomkabili na wenzake wawili wakikana mashtaka yao.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi umekamilika kwa mshtakiwa Shalaby na Benson na kwamba wanaomba kupangiwa tarehe nyingine.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Jumatano Agosti 11, 2021 na washtakiwa kurejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz