Kiungo wa klabu ya Simba, Clatous Chama Avunja Ukimya Kuhusu Sinto Fahamu yake na Mo Dewji - EDUSPORTSTZ

Latest

Kiungo wa klabu ya Simba, Clatous Chama Avunja Ukimya Kuhusu Sinto Fahamu yake na Mo Dewji


Kiungo wa klabu ya Simba, Clatous Chama amevunja ukimya kufuatia yale yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na majibu aliyojibiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji wakati alipokuwa akimsifia @hajismanara katika ukarasa wake wa Instagram.

“Kilichotokea jana ni drama (maigizo) ambazo hazikutarajiwa lakini kila kitu kipo sawa, kama nilivyosema namkubali/namheshimu kila mmoja anayeitakia simba mazuri bila kuwa na upendeleo au kushinikizwa.

“Watu wengi wanatamani kutuona tukigombana bila sababu, tusiwape maadui nafasi, sababu yoyote ya kutuharibu.

Read More: Nafasi za Ajira Serikalini na Mashiriki Binafsi Nimekuwekea Hapa  

“Tuna Ligi Kuu, ASFC (FA) za kutetea na Kazi ambayo hatujaimaliza ya kuchukua kombe la CAF, tuonane badae,” @realclatouschama

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz