Japan yasitisha matumizi ya dozi 1.6 za chanjo Moderna kuhusu hofu ya kuchanganywa na vitu visivyojulikana - EDUSPORTSTZ

Latest

Japan yasitisha matumizi ya dozi 1.6 za chanjo Moderna kuhusu hofu ya kuchanganywa na vitu visivyojulikana

Japani imesimamisha utumiaji wa dozi milioni 1.63 za chanjo ya Moderna kwa sababu ya kuchanganywa na ‘vitu visivyojulikana’.

Wizara ya afya ilisema "vitu vya kigeni" vilipatikana katika dozi kadhaa za takriban chupa 560,000 za chanjo hiyo.

Kampuni ya dawa ya Takeda, ambayo inauza na kusambaza chanjo hiyo huko Japan, ilisema Moderna ilikuwa imeshikilia shehena tatu "kama tahadhari ".

Ilisema suala katika eneo la utengenezaji nchini Uhispania ndio sababu inayolaumiwa kwa hali hiyo lakini haikufafanua.

"Hadi sasa, hakuna masuala ya usalama au ufanisi yaliyotambuliwa," Moderna ilisema, ikiongeza kuwa itashirikiana na wasimamizi na Takeda kuchunguza suala hilo zaidi.

Hakuna maelezo ya "vitu vya kigeni" ni nini, lakini Takeda iliielezea kama chembe chembe, baada ya hapo ilisema ilifanya uchunguzi wa dharura.

Ripoti za uchafuzi pia zilitoka kwa vituo vingine saba vya chanjo, kulingana na jarida la Japan Times, na dozi 390 - zilizopatikana zimeathiriwa.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz