Chui Amshambulia MREMBO wa Ujerumani Akipiga Selfie na Chui - EDUSPORTSTZ

Latest

Chui Amshambulia MREMBO wa Ujerumani Akipiga Selfie na Chui

 


Mwanamitindo aliye na umri wa miaka 36 -ameshambuliwa na chui baada ya tukio la kupiga picha katika makazi ya wastaafu yaliyotengwa kwa ajili ya maonyesho ya wanyama kugeuka kuwa mkasa Mashariki mwa Ujerumani.

Mwanamke huyo, anayeelezewa kuwa mpenda wanyama na masuala ya mitindo ulijeruhiwa vibaya kichwani ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni makazi ya chui wawili, Troy na Paris.


Polisi wanasema alipelekwa hospitali siku ya Jumanne akiwa na majeraha mabaya.


Tahadhari baadaye ilitolewa kwamba wanyama hao wametoweka lakini iliainika baadaye kwamba ni taarifa za uzushi.


Mamlala katika eneo la Burgenland zimesema hakuna hatari yoyote kwa wakazi na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini kilichotokea katika mkasa huo wa Nebra ikatika jimbo la Saxony-Anhalt.


Gazeti la Bild nchini Ujerumani lememtaja mwathiriwa kuwa Jessica Leidolph.


IHaijabainika alikuwa anapiga picha za nini na ninani aliyekuwa anaongoza mpango huo.


Kulingana na tovuti yake, Bi Leidolph anamiliki wanyama tofauti wakiwemo farasi, paka, njiwa na kasuku.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz