Breaking: Waziri Junior Aaga Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Breaking: Waziri Junior Aaga Yanga



Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wana Yanga kuanzia makocha, wachezaji, viongozi na mashabiki kwa kuniamini na kuwa mmoja wao. Haikuwa safari rahisi licha ya kuwa fupi mno.

Nilifika Yanga SC nikiwa na malengo makubwa lakini haikwenda kama nilivyotarajia labda kwa sababu zangu binafsi au vinginevyo. Ni kawaida yetu sisi wanasoka kukutana na changamoto kama hizi.

Nimechukua maumuzi mgumu sana kwangu lakini yote ni kwa maslahi mapana ya ufanisi wangu. Nimeona nihamishie jitihada zangu sehemu nyingine.

Yamkini sikufikia malengo ya klabu na kutokuwapa mashabiki ile furaha waliyotarajia kutoka kwangu lakini niwatoe shaka kuwa haikuwa dhamira yangu kuwaangusha.

Niwatakie kila la kheri kwenye safari yenu kuelekea msimu ujao. Tuendelee kuombeana labda ipo siku tutakuwa pamoja tena kama sio, basi nitaendelea kuuenzi upendo na imani mliyoijenga kwangu. Najivunia kuvaa nembo ya Klabu Kubwa hapa nchini. Asante (mungu kwanza). @wazir_junior_10.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz