Askofu Gwajima "Ninakwenda Kupasua Ukweli Bungeni Nitaonge Ambayo Hamjawahi Kusikia" - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Askofu Gwajima "Ninakwenda Kupasua Ukweli Bungeni Nitaonge Ambayo Hamjawahi Kusikia"Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dk. Josephat Gwajima amesema kesho tarehe 23 Agosti anakwenda kupasua ukweli mbele ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge baada ya kupokea barua ya wito wa kutakiwa kwenda kujieleza mbele ya kamati hiyo. Anaripoti Mwandishi wetu. (Endelea)…

Akizungumza mbele ya waumini wake leo Tarehe 22 Agosti, Askofu Gwajima amesema ameamua kuwaeleza umma kuhusu wito huo kwa kuwa aliyetoa barua hiyo ameisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema atakwenda mbele ya kamati hiyo na wategemee ukweli kama mojawapo ya imani ya CCM inavyosema kwamba ‘nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko’.

“Na nitaongezea mengine ambayo sijasema na mengine ambayo hamjasikia najazia. Ndio mtu wa Mungu anatakiwa kuwa hivyo, maisha yanatakiwa kuwa hivyo, lazima tusimamie nchi na watoto wetu.


“Ndio maana nasema namsapoti Rais, kamati ilisema watu wachanjwe au lah, na mimi nakuambia wewe kama rafiki yangu tumia hiyari yako uliyoambiwa uchanjwe au usichanjwe, sisi tumechagua lah.

“Kula matunda, fanya mazoezi, nenda kazini, ondoa uoga. Songa mbele, omba kwa dini yako. Mungu yupo hawezi kuacha tuondolewe namna hii,” amesema.

Jana tarehe 21 Agosti, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kupitia taarifa ambayo ilitolewa kwa umma, aliagiza Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa kufika mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwamo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya muhimili huo.


Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz