Vanessa Mdee akanusha kuzaa mtoto "Mmemshtua Mama Yangu" - EDUSPORTSTZ

Latest

Vanessa Mdee akanusha kuzaa mtoto "Mmemshtua Mama Yangu"Staa wa Tanzania anayeishi Marekani kwa sasa Vanessa Mdee, amevunja ukimya kuhusu taarifa za mitandaoni zikidai kwamba amejifungua mtoto na mpenzi wake Rotimi hali ambayo imempanikisha mama yake aliyepo Jijini Arusha.

Vanessa Mdee ametumia Insta Story yake baada ya kushea video clip iliyokuwa na ujumbe wa kukanusha taarifa hizo kwa kusema.

"Sina mtoto 'you freak my mom out' mama wa watu yupo zake Arusha mnaanza kumpanikisha kwamba nimezaa, aliyewaambia nimezaa ni nani".

Huu ni mwaka wa pili na Vanessa Mdee na Rotimi tangu waanze mahusiano yao na tayari wameshachumbiana lakini mashabiki wao wamekuwa wakitamani couple hiyo ipate mtoto.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz