Soko Kuu Mjini Mombasa Lateketea kwa Moto - EDUSPORTSTZ

Latest

Soko Kuu Mjini Mombasa Lateketea kwa Moto




Wafanyabiashara na wateja wako katika soko maarufu la Macknon mjini Mombasa. (Picha ya AFP)
Wafanyabiashara na wateja wako katika soko maarufu la Macknon mjini Mombasa. (Picha ya AFP)
Soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa nchini Kenya limepata hasara kubwa kutokana na moto ambao ulilikumba soko hilo Jumamosi usiku kuamkia Jumapili.

Wafanya biashara katika soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa wamepata hasara kubwa baada ya moto mkubwa kushuhudiwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili

Hakuna ripoti za maafa wala majeruhi kufikia sasa huku juhudi za kuzima moto huo zikiendelea.

Magari ya zima moto kutoka kitengo cha serikali za ugatuzi wakishirikiana na polisi wako kwenye tukio wakijaribu kudhibiti hali.


Wakati huu ambapo kuna sharti la kutotoka nje wakati wa usiku kwa sababu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, baadhi ya wakaazi wa maeneo ya karibu wako nje kushuhudia moto huo na wengine wakitoa msaada wa kudhibiti moto.

Hali hii imewalazimu maafisa wa kushika doria nyakati hizo kuweka usalama eneo hilo pia kuepusha visa vya uporaji kutokea kwenye baadhi ya maduka yaliyoachwa wazi kutokana na moto huo.

Haijabainika chanzo cha moto huo, na hakuna mwenye kufahamu nini hasa ilikuwa sababu ya moto.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz