Nani Kachoma Soko la Kariakoo, Mashuhuda Walalamika vifaa Duni - EDUSPORTSTZ

Latest

Nani Kachoma Soko la Kariakoo, Mashuhuda Walalamika vifaa Duni


KIKOSI cha zimamoto kimefanikiwa kuzima moto katika soko maarufu la Kariakoo jijini Dar es Salaam ambao umewaka na kuteketeza mali za thamani ya mabilioni kwa zaidi ya masaa tano.

Mamlaka zimesema zitafanya uchunguzi juu ya chanzo cha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea, lakini waangalizi na mashuhuda walishutumu teknolojia iliyotumika na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji pamoja na usimamizi wa soko.

"Soko halina vifaa vya kugundua moto wala halina vifaa vya kisasa vya kuzima moto," Joyce Moses, mfanyabiashara ambaye mali zake ziliteketezwa chini alilalamika. "Soko lina vizima moto vya kawaida na kwa sababu ya teknolojia duni nimepoteza kila kitu."

Haikuwa rahisi kuashiria ni nani aliwasha soko hilo. Lakini, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Elisa Mgisha aliwaambia waandishi wa habari kwamba kikosi hicho kiliarifiwa saa 2:40 usiku juu ya moto uliowaka sokoni. "Tulifika hapa kwa wakati shida pekee ambayo tulikabiliwa nayo ni uhaba wa maji kwani tulilazimika kuendesha gari kwenda na kurudi uwanja wa ndege ambako kuna bomba maalumu la maji," alisema.


Mgisha alifafanua kwamba moto ulianzia ghorofa ya juu (ghorofa ya pili) na uliongezeka na kufika chini. Alisema kikosi chake kwa kushirikiana na vikosi vingine na tulikuwa na magari 10 viliweza kutenganisha na kuokoa soko dogo la kariakoo lililokuwa karibu. Hadi saa 7: 40 usiku, karibu kila kitu ndani ya soko.

Msimamizi huyo wa vikosi vya uokoaji alikili kuwa kuna vizima moto katika soko na watu wamefundishwa jinsi ya kuvitumia, kwa bahati mbaya, soko lilikuwa limefungwa. "Vizima moto huhitaji wanadamu kufanya kazi," alisema na kushukuru timu ambayo imeweza kupambana na moto kwa saa nyingi katikati ya mazingira magumu ya kazi.

Komba Thabit Mwenyekiti wa eneo la Kariakoo anasema tukio hilo ni kubwa kuwahi kutokea na ni la kwanza ambalo amelishuhudia tangu kuanzishwa kwa soko hilo zaidi ya miongo minne iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala alitembelea soko hilo na kuagiza jeshi la polisi kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Haijabainika uharibifu unaohusishwa na tukio la moto lakini bidhaa zenye thamani ya mabilioni ya shilingi ikihusisha na mnyororo wa thamani zimeathiriwa.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz