Sintofahamu imetokea kwenye hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Bariadi ya Somanda baada ya familia ya Mayenga Nigonzala kulalamika kwenye vyombo vya habari kuwa ameshangazwa na kukabidhiwa mtoto mmoja licha ya kuwa vipimo vya awali vya ujauzito kuonesha mama huyo alikuwa na watoto mapacha tumboni.
Mama huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji mei 23 mwaka huu na amesema vipimo vya wakati wa mahudhurio ya kliniki na hata vile vya mwisho kabla ya kufanyiwa upasuaji huo vilionesha pia uwepo wa mapacha tumboni mwa mwanamke huyo.
"Nilipofika hospitali daktari aliyenipima aliniambia kwa umri wangu wa miaka 16 sitoweza kujifungua kawaida kwasababu watoto walikuwa wamechoka na wote wawili walikuwa wanataka kutoka kwa wakati mmoja."alisema Zawadi Sayi
Kwamujibu wa mzazi huyo ni kuwa muuguzi mmoja alimdokeza kuwa alijifungua mapacha na kuondoka akimuacha na sintofahamu.
Uongozi wa hospitali hiyo haukupatikana kwa njia ya simu kujibu tuhuma hizo. Familia hiyo inaishi katika kijiji cha Kidinda wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu
Post a Comment