Simba Bingwa! baada ya kuvuna point tatu kutoka kwa KMC - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Bingwa! baada ya kuvuna point tatu kutoka kwa KMC

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Didier Gomes  kimesepa na pointi tatu mazima mbele ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma KMC 0-2 Simba na kuwafanya mabingwa hao watetezi kuibuka wababe.

Inakuwa ni mara ya pili kwa msimu huu kwa Simba kusepa na pointi tatu mbele ya KMC kwa kuwa mchezo wa kwanza walishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Jumla Simba imesepa na pointi sita msimu huu mbele ya KMC.

Ni mabao ya Chris Mugalu dk ya 2 na 44 yalitosha kuipa pointi tatu Simba ambayo ilitoka kupoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

KMC ilishuhudia mabao yote kipindi cha kwanza jambo lililowafanya kipindi cha pili kuongeza umakini kwa kuwa hawakuruhusu bao.

Beki wao Andrew Vincent alitolewa kipindi cha pili kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Sasa Simba inafikisha pointi 76 ikiwa na uhakika wa kutwaa ubingwa wao kwa kuwa pointi hizo zinaweza kufikiwa na Yanga ila tatizo itakuwa katika idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba imefunga jumla ya mabao 71 huku Yanga ikiwa imefunga jumla ya mabao 50 imecheza mechi 32 na imebakiza mechi mbili wakati Simba imecheza mechi 31 na imebakiza mechi tatu.

KMC inabaki nafasi ya sita na pointi 42 baada ya kucheza jumla ya mechi 32 ndani ya ligi.
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz