'Sikuwahi Kuwa na Urafiki Nao' Mavoko Azungumzia Uhusiano na Diamond & Harmonize, Ataja Sababu za Kuondoka Wasafi - EDUSPORTSTZ

Latest

'Sikuwahi Kuwa na Urafiki Nao' Mavoko Azungumzia Uhusiano na Diamond & Harmonize, Ataja Sababu za Kuondoka Wasafi
Staa wa Bongo Rich Mavoko amekiri kuwa hajawahi kuwa na urafiki na bosi wa Wasafi Diamond Platinumz wala Harmonize.

Mavoko ambaye alijitoa Wasafi miaka mitatu iliyopita amesema kuwa hajawahi kutana na wawili hao tangu agure Wasafi.

Akizungumza na Massawe Japanni kwenye kitengo cha 'Ilikuaje?', Mavoko alieleza kuwa uhusiano wake na waliokuwa nao Wasafi ulikuwa wa kibiashara tu ila hawakuwa marafiki.


"Hatujawahi kutana naye(Diamond".. mimi niko sawa. Wote tuko nao sawa ila hatujawahi kutana nao (Diamond na Harmonize). Inabidi watu watofautishe urafiki na biashara, sikuwahi kuwa rafiki na hao watu, nilikuwa nafanya biashara pale. Kabla hata niende Wasafi, nilikuwa nafanya muziki pekee yangu. Sikuwahi kuwa na urafiki na Diamond , aliponihitaji tufanye kitu pamoja, mimi nilifanya kama biashara sio urafiki" Mavoko alisema
Nafasi za Ajira Serikalini Bonyeza HAPA

Nafasi za Scholarships Bonyeza HAPA

Nafasi za Internships Bonyeza HAPA

Alipoulizwa sababu zilizompelekea kuondoka Wasafi, mwanamuziki huyo alitaja kuwa kulikuwa na tofauti za kibiashara ila akasita kufafanua zaidi kuhusu mzozo ambao uliibuka. Alisema kuwa alitaka kufanya muziki wake kama alivyotaka mwenyewe.

"Watu wanahitaji kuelewa kuwa ile ni biashara. Ikifika kipindi nione nataka kufanya biashara yangu vile ninavyotaka na naona nashindana na wewe hamna haja ya kugombana ninaweza kuondoka. Ni biashara tu hamna kitu kibaya" Alisema Mavoko

Mavoko alisema kuwa hakuna utofauti wowote ambao ulitokea baada yake kuondoka pale
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz