Shahidi: Walituvamia Dukani, Sabaya Alikuwa Akitoa Amri Zote - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Shahidi: Walituvamia Dukani, Sabaya Alikuwa Akitoa Amri Zote
SHAHIDI wa pili katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, Numan Jasin (17) amewatambua kwa kuwashika mabegani Sabaya na wenzake.

 

Shahidi huyo ametoa ushahidi huo leo Alhamisi, Julai 22, 2021, Mbele ya Hakimu Mkazi, Odira Amworo amesema Sabaya ndiye alikuwa anatoa amri zote, huku mshitakiwa wa pili alimpa simu kutaka apige nyumbani kufungua milango na wa tatu walikaa naye kwenye gari.

 

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka shahidi huyo amesema awali wakiwa dukani hakuweza kuwatambua kwani kulikuwa na vurugu dukani.

 

Shahidi huyo amesema watuhumiwa hao waliwaweka chini ya ulinzi kwa takriban saa tatu kuanzia saa 11 jioni, walipigwa, kusachiwa na kuhojiwa na watuhumiwa hao. Amesema katika duka hilo walikuwa chini ya ulinzi watu nane, ambao ni yeye, mjomba wake Hajirin Saad, Ally, Mzee Salimu, Annas, Abuu Mansoor, Bakari Msangi na msichana mmoja.

 

Jasin amesema baada ya kuwa chini na ulinzi baadaye, waliachiwa wenzao na alibaki yeye na mjomba wake ambao walitakiwa kupanda katika gari lililokuwa nje ya duka. Hata hivyo amesema mjomba wake ambaye alikuwa amefunga aliomba kununuliwa ndizi ili afungue ndipo Sabaya aliwanunulia ndizi moja moja.

 

Amesema baada ya kuondoka dukani magari yaliwapeleka nyumbani ambapo walikuta milango imefungwa ndipo alipewa simu kumpigia mama yake na aliongea na kiarabu kumtaka asifungue.

 

Amesema baadaye walipelekwa kituo cha polisi Arusha na waliandika maelekezo na kupewa dhamana hadi Februari 10 saa 10 jioni. Amesema kwa kuwa walimaliza mahojiano usiku polisi aliyekuwa anawahoji aliwapa msaada wa gari lake kuwarudisha nyumbani.
Shahidi huyo wa pili anaendelea kutoa ushahidi wake.

 


Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz