China yakataa WHO kuchunguza mara ya 2 chanzo cha COVID-19 - EDUSPORTSTZ

Latest

China yakataa WHO kuchunguza mara ya 2 chanzo cha COVID-19China imesema haitawaruhusu maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO wa kufanya awamu ya pili ya uchunguzi kuhusu chanzo cha maradhi ya COVID-19 kwenye maabara za nchini humo. 
Naibu mkuu wa tume ya kitaifa ya afya nchini China Zeng Yixin amesema hayo hii leo na kuongeza kuwa ni mpango wa WHO umejaa lugha ambayo haiheshimu misingi ya sayansi huku akipuuzilia mbali nadharia kwamba virusi hivyo vilitokea kwenye maabara za Wuhan mji ambako viligunduliwa kwa mara ya kwanza. 

Wameongeza kusema kuwa maabara hizo hazina virusi vinavyoweza kumuathiri mwanadamu moja kwa moja.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz