Sababu Lamine Kuvunjiwa Mkataba Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Sababu Lamine Kuvunjiwa Mkataba YangaIMETAJWA nidhamu ndiyo sababu iliyomuondoa nahodha na beki wa kati wa Yanga, Mghana, Lamine Moro kwenye usajili wa msimu ujao.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu, uongozi wa Yanga utoe taarifa za kuachana na beki huyo mwenye umbo kubwa.

Moro anaondoka Yanga akiwa amecheza michezo 21 katika Ligi Kuu Bara akifunga mabao 4 huku akipiga asisti moja pekee.Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa, beki huyo hakuachwa na timu hiyo kutokana na kiwango, bali nidhamu ndiyo iliyomuondoa katika timu.

Bosi huyo alisema kuwa Moro hivi karibuni alitofautiana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi katika suala la nidhamu kabla ya kuondoa kambini Ruangwa, Lindi wakati Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya Namungo FC.Aliongeza kuwa beki huyo alitenda utovu wa nidhamu lakini akaonekana mgumu katika kuomba msamaha kwa kocha huyo.

“Uongozi wa Yanga umefikia uamuzi wa kuachana na Moro baada ya kuitumikia kwa mwaka mmoja na nusu huku akiwa mkali.“

Hatua hii ya kusitisha mkataba wa beki huyo haitokani na kiwango chake, bali ni kitendo chake cha kutofautiana na kocha wetu Nabi pamoja na kuyumba kwa nidhamu yake hivi karibuni ndio kimepelekea kuvunjiwa mkataba.“

Katika makubaliano hayo Yanga na Moro wamekubaliana watalipana mshahara wa mwezi mmoja pekee ambao ni wa Agosti pekee tofauti na huu wa Julai unaomalizika alioutumikia katika timu,” alisema bosi huyo.Yanga jana ilitoa taarifa rasmi kutoka kwenye idara ya habari ya timu hiyo ikitangaza kuachana na beki huyo.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz