Ndege tumezipata kwa jasho na damu- Rais Samia - EDUSPORTSTZ

Latest

Ndege tumezipata kwa jasho na damu- Rais SamiaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amelitaka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kuzitunza ndege zinazonunuliwa na serikali kwa kuhakikisha linadhibiti hujuma kwa ndege hizo ili ziweze kuleta tija.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Julai 30, 2021, wakati wa mapokezi ya ndege mpya aina ya Bombadier Dash 8 - Q400, ikiwa ni ndege ya 9 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na serikali.

"Wito wangu kwenu Ndege hizi tumezipata kwa jasho na damu, nataka niwaombe watumishi wa shirika kuwa makini katika utunzaji na uhudumiaji wa ndege hizi tunazozinunua, kiufupi kudhibiti vitendo vya hujuma kwa ndege zetu zikitunzwa zitakaa kwa muda mrefu na kuleta tija iliyokusudiwa," amesema Rais Samia.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz