Mwanamke achoma moto nyumba amuua mpenzi wake Mbezi Makabe - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamke achoma moto nyumba amuua mpenzi wake Mbezi MakabeMwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Khamisi maarufu (Zungu), amefariki dunia baada ya mpenzi wake Neema Mushi waliokuwa wanaishi naye Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam, kuchoma moto nyumba hiyo na kusababisha kifo kwa kile kinachodaiwa wamepishana kauli, huku fremu za wafanyabiashara zilizokuwa kwenye nyumba hiyo kuteketea moto.

Kwa Mujibu wa Mwandishi wetu Juma Kapalatu aliyefika kwenye nyumba hiyo ambayo kijana huyo alikuwa anaishi na mpenzi wake, ametueleza kuwa nyumba hiyo mmiliki mkubwa ni Neema ambaye alikuwa akiishi na bwana Khamisi, ambapo jeshi la polisi limefika na kuchukua mwili wa kijana huyo.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz