Mo Dewji Asimulia Kwa Mara ya Kwanza Alivyotekwa – “Waliniwekea Bastola, Nilihisi Nakufa” - EDUSPORTSTZ

Latest

Mo Dewji Asimulia Kwa Mara ya Kwanza Alivyotekwa – “Waliniwekea Bastola, Nilihisi Nakufa”
Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘MO Dewji’ Julai 24, 2021 amekutana na waandishi wa habari kuzungumza kuhusu maendeleo ya Foundation yake, sasa miongoni mwa aliyoyazungumza mbele ya waandishi ni kuhusu sakata lake la utekwaji.


“Lakini lazima nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu lakini pia nina deni kubwa sana na nchi hii kwani mnajua nilitekwa niliwekewa mabunduki”


“Nilifungwa macho siku tisa nilikuwa najua nitakufa lakini dua awe Mkristo ama Muislamu ama awe Chama cha Mapinduzi watu wameniombea sana”


“Wapi umeona Duniani kwamba mtu masikini anamuombea mtu tajiri ulishawahi kusikia wapi, lakini watanzania wameniombea kwa imani zao zote nina deni”


“Naipenda nchi yangu nitakufa hapa nitazikwa hapa hapa kwa hivyo namshukuru Mwenyezi Mungu lakini pili pia nimshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ametuletea mwelekeo mpya na watu watapata ajira Serikali itapata kodi tumeanza kufanya mahusiano mazuri na Dunia nzima” amesema Mo Dewji

Taasisi ya Mo Dewji imewekeza zaidi ya TSh Billioni 1 kwenye Programu ya Udhamini wa Mo ambayo inasaidia wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali Tanzania kupitia Vyuo Vikuu. Tumesaidia zaidi ya wanafunzi 100 ambao ni wanasayansi, walimu, wahandisi, wachumi, wanaisimu na wajasiriamali!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz