Mavoko Afichua Siri "Diamond Platnumz Hakuwa Rafiki" - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mavoko Afichua Siri "Diamond Platnumz Hakuwa Rafiki"Msanii wa Bongof Fleva, Rich Mavoko amedai kuwa hakuwahi kuwa na ushikaji wala urafiki na Diamond Platnumz licha ya kusainiwa kwenye lebo yake, WCB Wasafi.

Akihojiwa na Willy M Tuza kwenye kipindi cha Mambo Mseto kinachoruka Radio Citizen, Kenya, Mavoko amesema hata kujiunga kwake kwenye lebo hiyo ni Diamond alimtumia watu.

"Hatukuwa kuwa washikaji, na hata tulipokuwa kwenye lebo hatukuwahi kuwa marafiki," amesema Mavoko ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake mpya, Nidonoe.

"Sikuwahi kumtafuta mtu kufanya naye kazi kwa sababu nilikuwa na kipaji sana. Nilitafutwa na watu wengine ambao yeye aliwatuma, alishindwa kuni-face, I think," amesema Rich Mavoko.

Pia Mavoko amesema licha ya kutamba na kuwa msanii mkubwa kabla ya kusaini WCB Wasafi, si sawa kushindanishwa na Diamond kwani wakati anatoa albamu yake ya kwanza, Kwamwambie (2010) yeye alikuwa Kidato cha Nne, hivyo wamepishana kiumri ndani ya muziki.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz