Manara asitisha kuongea na wanahabari - EDUSPORTSTZ

Latest

Manara asitisha kuongea na wanahabariMkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Manara, amesema hatoongea lolote kama alivyoahidi juma lililopita.

Manara alitoa ahadi ya kuongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari, kufuatia sakata lake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez.

Manara ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa: Kuanzia Siku ya Jumatano hadi leo ndizo siku nilizoongea na simu nyingi zaidi na kwa muda mrefu pengine kuliko Siku zote za maisha yangu..
Lakini WhatsApp na DM ndio ilikuwa balaa, hapo usiniulize SMS na E-mail.

Yes kila mmoja akiniambia lake , kiukweli nimewasikia na kama Binadaam acha tungoje asili ichukue nafasi yake.


 
Mwenyekiti wa Simba HQ Farouk Baghoza TSN , Mbunge na Mwanachama wetu maarufu Mh @jmakamba , Makamu Mwenyekiti wa Bodi Salim Try Again , ambao tumefanya conference calls nyingi na wote wengine nimewaelewa.

Sitaongea lolote Kwa sasa nikiamini katika maslahi makubwa ya Simba, team ya maisha yangu.

Captain wangu @john_22_bocco always naamini ktk ww linapokuja Nahodha wa mfano, tuliongea nikiwa ktk bad mood lakini nasaha zako na Kwa heshma ya jana ninakataaje Kwa mfano kukusikiliza?

Washabiki wote wa Simba na Waandishi mliokuwa na hami na press yangu Am Sorry , acheni Ibilisi aepukwe ngoja tusubiri mchanga wa Pwani.

Kimsingi nimemaliza sina lingine ila walioumia Kwa ajili ya Simba ,again poleni na Samahani.

Kwa wale akina sie niwaambie ndoo ya maji haijazwi upepo

Af’wan 🙏
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz