Maelekezo ya ada kidato cha 5 haya - EDUSPORTSTZ

Latest

Maelekezo ya ada kidato cha 5 haya 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wakuu wa shule zote za serikali kutoza michango ya kujiunga na kidato cha tano zaidi ya Sh. 188,000.

Amesema mkuu yeyote wa shule atakayebainika kukiuka agizo hilo, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Ummy alitangaza katazo hilo jana alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma kukagua utayari wa shule za serikali kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2021.

Alisema kiasi hicho kinajumuisha ada ya Sh. 70,000.

Waziri Ummy alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa mwaka huu ni 87,663 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule 476 na kutoa wito kwa wazazi ambao wataamua kuwapeleka watoto wao kwenye shule za binafsi kutoa taarifa kupitia mfumo, ili kutoa fursa kwa wengine.


 
Aidha, aliwataka wakuu wa shule kuandaa mazingira mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwapo na mahitaji yote muhimu.

Aliwataka wanafunzi wa bweni kuripoti Julai 3 na wa kutwa Julai 5.

Kadhalika, alisema katika ajira mpya za walimu hivi karibuni hakuna shule itakayokosa mwalimu wa Fizikia wala Hisabati.


Alifafanua kuwa walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 wakati shule ambazo hazikuwa na mwalimu ni 1,100 na walimu wa Hisabati walioajiriwa ni 459 wenye shahada na stashahada 140 wakati uhaba ulikuwa kwa shule 400.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz