China yashutumiwa kwa udukuzi wa Kimataifa - EDUSPORTSTZ

Latest


 

China yashutumiwa kwa udukuzi wa KimataifaNchi ya Marekani na washirika wake, wameishutumu China kwa kuendesha kampeni ya kimataifa ya upelelezi wa mitandaoni.Marekani iliungana na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Umoja wa Ulaya, Australia, Uingereza, Japan, Canada na New Zealand katika kulaani udukuzi huo, ambao Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema unaweka kitisho kikubwa kwa usalama wa kiuchumi na kitaifa.

Sambamba na hilo, Wizara ya Sheria ya Marekani imewashitaki raia wanne wa China, maafisa watatu wa usalama na mtaalamu mmoja wa udukuzi, kwa kuzilenga kampuni, vyuo vikuu na mashirika ya serikali nchini Marekani na kwingineko ulimwenguni. Msemaji wa ubalozi wa China mjini Washington Liu Pengyu, aliziita tuhuma hizo dhidi ya China kuwa za kijinga.

By-BAKARI WAZIRI


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz