Binti wa Monalisa Apata ‘Divisheni One’ Kidato Cha Sita - EDUSPORTSTZ

Latest

Binti wa Monalisa Apata ‘Divisheni One’ Kidato Cha SitaMsanii mpya wa Bongo Fleva, Sonia Monalisa ambaye ni binti wa staa wa Bongo Movies, Monalis aamepata ‘divisheni one’ katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotoka jana.

Mrembo huyo alikuwa anasoma Shule ya Tusiime ya jijini Dar.

Ikumbukwe kwamba, hata kidato cha nne alimaliza shuleni hapo na kupata divisheni one ambapo pia kwenye mahafali yao alizawadiwa baada ya kuibuka mwanafunzi bora kwenye masomo mengi mno na mitihani ya Taifa ya kidato cha nne alitajwa kupata A karibia masomo yote hadi hesabu linalowatoa jasho wengi.Kwa upande wa mama yake, Monalisa amempongeza binti yake huyo maarufu kwa kusema haikuwa kazi rahisi kwani wakati wa kipindi cha kufanya mitihani ya kidato cha sita kwani Sonia alikumbwa na changamoto f’lani kubwa.

 

“Haleluya, Mungu wangu ni mwema. Ahsante Mungu wangu. Ahsante mwanangu Sonia kwa kutupatia matokeo mazuri, tangu mchana nilipopata matokeo sijielewielewi; yaani maana najua wakati mgumu uliopitia kipindi cha mitihani. Ilikuwa ni mtihani mkubwa, lakini yote ni shetani na ameshindwa in Jesus name.

Ahsante walimu wote wa Tusiime kwa miaka sita 6 ya bidii. Ahsante pia, division 1 safiiiiiiiiiiiiiiii”

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz