Rais Samia:Nchi imekumbwa na Wimbi la Tatu la Corona - EDUSPORTSTZ

Latest

Rais Samia:Nchi imekumbwa na Wimbi la Tatu la Corona




RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema tayari nchi imekumbwa na wimbi la tatu la ugonjwa wa COVID-19 na kwamba wagonjwa wa ugonjwa huo wapo na kuwaomba viongozi wa dini kuwakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kujikinga na ugonjwa huo, ili Taifa liweze kujiepusha na vifo vya makundi makundi.

 

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 25, 2021, mkoani Dar es Salaam, alipokutana na kuzungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini (TEC), ambapo ametumia nafasi hiyo pia kuwaomba viongozi wa dini nchini kutoa elimu ya kujikinga kwa waumini wao ikiwemo kuwasisitiza kuchukua tahadhari na kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa afya.

 

“Sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika hili wimbi la tatu, kama mnakumbuka siku nimetembelea hospitali ya Mwananyamala daktari aliniambia kuna wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua,“ alisema Rais Samia.

 

Rais Samia ameongeza kwa kusema”Daktari nikamuambia ni COVID-19 akasema ndiyo, wakati wapiga picha wangu walikuwa wamekwishatangulia nikawaambia ninyi ebu tokeni haraka huko, hili jambo lipo, tunawaomba sana viongozi wa dini mliseme hili kwa waumini ili tujiepushe na vifo vya makundi”.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz