Mtoto wa Kajala Paula Azidi Kujilipua Instagram - EDUSPORTSTZ

Latest

Mtoto wa Kajala Paula Azidi Kujilipua InstagramHAKAMATIKI!Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mtoto wa muigizaji Kajala Masanja, Paula kuwa na mwendelezo wa matukio ya kujilipua kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram unaokwenda kwa jina la therealpaulahkajala, binti huyo aliyeishia kidato cha nne katika masomo yake, amekuwa akitupia picha zake za mitego mitego ambapo alianza kwa kuonesha kitovu chake.

Ukiangalia kwenye ‘page’ yake, Paula alikuwa akiweka picha nyingi za kitovu nje lakini akiwa amevaa nguo ndefu ila juzikati ndio kafanya balaa zaidi kwa kuposti picha akiwa amevaa kikaptula kifupi sana na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi.Paula ametupia picha kadhaa zikimuonesha akiwa na kikaptula hicho akiwa ameshika nanasi. Lakini pia mbali na hizo, zipo nyingine ambazo amepiga akiwa na kikaptula kilichombana na kuacha sehemu kubwa ya tumbo lake wazi.

“Mh! Huyu mtoto jamani shule ndio hamna tena hapa na mama yake amesharidhia haya mambo ndio maana anajilipua tu kila kukicha,” alichangia mdau mmoja kwenye mtandao wa Instagram.

Safari ya Paula kuanza kujilipua ilianza miezi kadhaa iliyopita baada ya kuingia kenye skendo ya kudaiwa kuvujisha picha za utupu za aliyekuwa mpenzi wa mama yake, Rajabu Abdul ‘Harmonize’.Kabla ya ishu hiyo, ilitangulia nyingine ya picha za kimahaba za Paula akiwa na staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’.Baadaye Rayvanny amejilipua tena kwa kuweka picha yao kwenye ukurasa wake wa Instagram wakiwa hotelini hivyo watu kujiongeza tu kwamba sasa hivi penzi lao si siri tena.

Baadhi ya wadau kwenye mitandao ya kijamii wamemuonya Kajala kusimamia maadili ya mwanaye huyo lakini wengine wakisema aachwe alee mwanaye vile anavyoona inafaa.

STORIMWANDISHI WETU, RISASI

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz