Mchekeshaji Jol Master Amuumbua Boss Wake Coy Mzungu Kisa Nyumba Mbaya - EDUSPORTSTZ

Latest

Mchekeshaji Jol Master Amuumbua Boss Wake Coy Mzungu Kisa Nyumba MbayaKIMEUMANA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mchekeshaji Jol Master kumuumbua laivu Bosi wake, Coy Mzungu, kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jol Master ameweka kipande cha video alichojirekodi akisikika akimchana Mzungu kuwa nyumba yake ni mbaya licha ya kuwa ana gari zuri lenye rangi ya zambarau ambalo ni ‘mtama kwa watoto’.

“Ifike mahali watu tuongee ukweli, ifike mahali waseme ukweli Coy nyumba yako ni mbaya, gari yako ni nzuri sana, gari ni nzuri lakini nyumba ni mbaya…” alisikika Jol Master.

Jol Master amemchana Mzungu ambaye ni bosi wa kipindi cha CHEKA TU, baada ya kufukua moja ya picha zake aliyoposti kwenye ukurasa wake wa Instangram ikimuonesha akiwa amepozi mbele ya kijumba chake ambacho kinaonekana rangi yake ‘imechoka’ na sehemu zingine za kuta zikiwa zina ‘mabonde mabonde’😁. We unamchukuliaje Jol Master kumkejeli bosi wake hivi?….

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz