Jela Kwa Kuua, Kumla Nyama Mama’ke - EDUSPORTSTZ

Latest

Jela Kwa Kuua, Kumla Nyama Mama’keAlberto Sanchez Gomez mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa mwaka 2019 baada ya maofisa wa Polisi kupata mabaki ya mwili katika nyumba ya mama’ke huku mengine yakiwa katika plastiki.

 

Jamaa huyo, raia wa nchini Hispania amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mamake na kumla nyama huku akikutwa na mabaki ya mwili wake.

Mahakama ilikataa kwamba alikuwa anakabiliwa tatazo la kiakili wakati wa mauaji hayo.Atatumikia kifungo cha miaka 15 kwa mauaji na miezi mingine mitano kwa uharibifu wa mabaki ya mfu. Pia ametakiwa kulipa faini ya Dola za Kimarekani 73,000 kama fidia.

 

Maofisa wa Polisi waliwasili katika nyumba ya mama yake huyo Februari, 2019 baada ya rafiki wa jamaa huyo kuwasilisha malalamiko juu ya mauaji ya Maria Soledad Gomez ambaye alikuwa na umri wa miaka 60.

 

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mahakama ilielezewa kwamba Sanchez, wakati huo akiwa na umri wa miaka 26 alimyonga mama’ke wakati wa mzozo.

Baadaye aliukatakata mwili wa mamake na kuula huku vipande vingine akiwalisha mbwa.

Vyombo vya habari vya Hispania vinasema kwamba alikuwa anajulikana na maofisa wa Polisi kutokana na ghasia dhidi ya mama’ke na kwamba alikuwa amekiuka agizo la kumkamata wakati alipokamatwa.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz