Je Wasanii Kuonesha Hela zao ni Ushamba? - EDUSPORTSTZ

Latest

Je Wasanii Kuonesha Hela zao ni Ushamba?Sio mara moja @diamondplatnumz akipost picha au video akitoa hela tu utasikia jamaa mshamba sana, jamaa anapenda sana kujionyesha na Comment nyingi zinasema mshamba.

Nikaona kidogo niwaletee baadhi ya watu maarufu Dunia, Wasanii maarufu na matajiri Afrika wakionyesha hela.

Hapo yupo Davido, Wzikid, Mayweather pamoja na Soulja Boy wakiwa wameshikilia maburungutu ya pesa ila wao wala hawasemwi washamba. Jamani eeeh kumbukeni hawa Celebrities ndio maisha yao. 

Kama msanii wako hajapost basi ni yeye na hulka yake ila ni swala la kawaida kwa wasanii kufanya hivo na sio kwamba ni ushamba ndio umaarufu wenyewe.

Punguzeni kulalamika jamani nyie mnajenga nyumba na munapost Facebook, mkinunue baiskeli au kula kuku munapost ila akipost Escalade Tatizo akipost HELA tatizo nyie mnataka apost nini jamani?? Akigawa misaada bado utasikia mkono wa pili usijue.

By Mdau
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz