Mapenzi Fanya Kwa Afya, Siyo Kujiumiza! - EDUSPORTSTZ

Latest

Mapenzi Fanya Kwa Afya, Siyo Kujiumiza!


 Ni Ijumaa nyingine nzuri ambayo Mwenyezi Mungu ametujaalia, hivyo hatuna budi kumshukuru kwa kila jambo.

Rafiki yangu, katika hali ya kawaida, kufanya tendo la ndoa kuna faida nyingi. Lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi, tunapata matatizo ambayo huleta madhara makubwa.

 

Kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kulala bila kufanya tendo huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu!

 

Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mmoja, lakini uchunguzi unaonesha kuwa, wengi baadaye hujikuta wakilalamika kupoteza hamu ya tendo.

 

Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa, anaweza kukabiliana nayo, ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya tendo kila tunapokutana. Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina;

 

KUPOTEZA HAMU YA TENDO

Watu wenye pupa za kufanya tendo, hupoteza haraka hamu ya mapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona mtupu.

 

Kukinai haraka staili za ufanyaji tendo, kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara nyingi kwa staili zilezile na pengine mazingira yaleyale; kitanda kimoja na chumba kilekile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya, hivyo kupoteza hamu na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

 

KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA

Tabia ya kufanya tendo mara kwa mara, huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa, hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye tendo na kwa wakati gani?

 

Watu wanaojiendekeza katika kufanya tendo mara kwa mara, ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani, humtamani bila kujali hadhi yake.

Hawa ndiyo wale wanaobaka, kusaliti hata kwa watumishi wa ndani au kufanya tendo na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya ngono.

 

Unapokuwa mtu wa kufanya tendo mara kwa mara, huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa. Mumeo akiondoka siku mbili, unatamani kuwa hata na ‘hausiboi’ ili akukate kiu.

 

KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO

Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na

kiu ya kufanya mapenzi, hivyo ukiwa mtu wa kufanya tendo kila mara, unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa.

Kama ni tendo, utakuwa unalifanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!

 

KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI

Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya tendo mara kwa mara, ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

Kama tujuavyo, tendo la ndoa hasa kwa wanaume, huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke.

 

Aidha, lishe inapokuwa duni, mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

Sambamba na hilo, mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya tendo mara kwa mara, huwa dhaifu.

 

KUPATA MAGONJWA

Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya tendo mara kwa mara, huwa na tamaa na hujikuta wanafanya tendo holela, jambo ambalo linaweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi, lakini ufanyaji wa tendo usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake, huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao nyeti kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana, hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo

Ukimwi. Mwisho nakushauri kufanya tendo la ndoa kwa afya na siyo kujiumiza.

Kwa leo naishia hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine murua.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz